Furahia Ladha Nzuri ya Juisi za Matunda Zenye Ubora wa Juu Kutoka Ulaya

“Juice your way” ni kampeni ya miaka mitatu, inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), ambayo inalenga kukuza juisi za matunda za Ulaya katika masoko ya Kenya na Uganda.
Lengo kuu la kampeni hiyo ni kuongeza ufahamu kuhusu ubora wa bidhaa za kilimo za Ulaya na viwango vya juu vinavyotumika wakati wa taratibu za uzalishaji na usindikaji katika EU na pia kuimarisha ushindani wa sekta ya kilimo ya EU.
Hasa zaidi, kampeni hii inalenga kukuza juisi za matunda na hasa juisi ya machungwa kutoka Ulaya ambayo ina sifa za kipekee tukizingatia ubora, usafi na ladha, na inazalishwa nchini Ugiriki.

Moja kwa moja kutoka shambani hadi kwenye glasi yako!

Hatua iliyopendekezwa iliwasilishwa na Muungano wa Vyama vya Ushirika vya Kilimo vya Argolis – REA. REA ni zao la Muungano wa Vyama vya Ushirika vya Kilimo vya Argolis, ilioanzishwa mwaka wa 1937. UAC ya Argolis – REA ndilo Shirika kubwa zaidi la Wazalishaji katika sekta ya matunda na mboga nchini Ugiriki, linaloshirikisha wanachama 786. UAC ya Argolis – REA ni Shirika linalotambulika la Wazalishaji katika sekta ya matunda na mboga nchini Ugiriki tangu 2013 na utambuzi wake unahusu matunda ya jamii ya chungwa (machungwa, mandarini, zabibu) na parachichi mbichi za kusindika, yaani kukamua juisi. Shughuli za UAC ya Argolis – REA zinalenga usindikaji wa mazao ya kilimo, hasa juisi ya matunda ya jamii ya chungwa na matunda mengine, upakiaji wa matunda na mboga pamoja na utoaji wa huduma za kilimo.